Marekani kuiondoa Sudani katika orodha ya nchi zinazofadhili Ugaidi

Nchi ya Sudani imefurahishwa na taarifa iliyotolewa na Marekani ya kuiondoa Sudani katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi

Marekani kuiondoa Sudani katika orodha ya nchi zinazofadhili Ugaidi

Nchi ya Sudani imefurahishwa na taarifa iliyotolewa na Marekani ya kuiondoa Sudani katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Sudan inasema, Kitendo cha Marekani kuiondoa Sudan katika orodha ya nchi zinazosaidia Ugaidi na kuwa tayari kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi kimewafurahisha.

Uongozi wa rais Donald Trump umetangaza kuiondoa Sudan katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. 

Kuhusiana na mada hii  msemaji wa  wizara ya mambo ya nje wa Marekani Heather Nauert alisema naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Sullivan na waziri wa mambo ya nje wa Sudani Ed-Derdiri Muhammed Ahmed walikutana jijini Washington na kuzungumzia kuanza kwa awamu ya pili ya mahusiano baina ya mataifa hayo.

Alisema watashirikiana na Sudan katika vita dhidi ya ugaidi, wataendeleza uhuru wa kuabudu na uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na misaada kwa jamii. vita vya ndani vitasimamishwa pamoja na kuweka mazingira mazuri ya mazungumzo ya amani ndani ya nchi hiyo.

Aliendelea kusema Nauert kwamba kama Sudan ikiendelea na kazi nzuri ya kuimarisha demokrasia, na kutekeleza masharti yote ya awamu yliyowekwakwenye awamu ya pili, Marekani iko tayari kuiondoa Sudani katika nchi zinazo fadhili Ugaidi.

 Habari Zinazohusiana