Hatimaye Muhammed Dewji apatikana

Mfanyabiashara biiionea wa nchini Tanzania ambaye alitekwa na watu wasiojulikana hatimaye apatikana akiwa salama

Hatimaye Muhammed Dewji apatikana

Mfanyabiashara na bilionea kijana  kutoka Tanzania, Muhammed Dewji maarufu kama Mo ambaye Alkhamisi iliyopita alitekwa na watu wasiojulikana amepatikana akiwa hai na mzima wa afya.

Katika ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa kampuni yake, amesema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani".

Nawashukuru watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao.

Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama."Habari Zinazohusiana