Jeshi la Polisi lazuia mkutano wa upinzani mjini Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Jeshi la Polisi lazuia mkutano  wa  upinzani mjini  Lubumbashi  Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

Kongo.jpg

Jeshi la Polisi Jumamosi  Lubumbashi limezuaia upinzani kukutana ambapo taarifa zimefahamisha kuwa mkutano huo lengo lake ilkuwa kupinga  mashne za uchaguzi ambazo zinatarajiwa kutumiwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika ifikapo Disemba 23 mwaka 2018.

Mkutano huo ulikuwa umeruhusiwa na baadae kupigwa marufuku na ofisi za meya wa jiji la Lubumbashi. 

Ofisi ya meya wa Lubumbashi ilitoa tangazo ambalo limesema kuwa mkutano huo utafanyika wakati ujao bila  ya kufahamisha tarehe. Mkutano huo umeahirishwa kwa sababu za kiusalama tangazo liliendelea kufahamisha.

Shirika la habari la Anadolu limefahamisha Jumamosi kuwa  makaazi ya Gabriel Kyungu ambae ni kiongoni wa upinzani Kusini-Mashariki mwa JK Kongo yalikuwa yamezingirwa na jeshi la Polisi.

Wafuasi wa upinzani walijaribu kujikusanya karibu na eneo ambalo kulikuwa kunatarajiwa kufanyika mkutano walishambuliwa kwa mabomu ya kusababisha kutokwa na machoni na risasi za moto.

Waziri mkuu wa zamani Adolph Muzito, mgombea wa kiti cha urais, Martin Fayulu na katibu wa chama cha MLC Eve Bazaiba walizuiliwa na Polisi kufika katika eneo lililokuwa limepangwa kufanyika mkutano.Habari Zinazohusiana