Maporomoko ya ardhi yasababisha maafa nchini Uganda

Watu kadha wafariki katika maporomoko ya ardhi katika mji wa Bukalasi nchini Uganda

Maporomoko ya ardhi yasababisha maafa nchini Uganda

Watu kadhaa wamefariki katika maporomoko ya ardhi katika mji wa Bukalasi wilaya ya Bududa nchini Uganda.

Timu za uokoaji zillikuwa zikijaribu kutafuta manusura na watu walioathirika kwa kutoa matope katika janga lililotekea alhmisi iliyopita katika mji wa Bukalasi wilaya ya Bududa nchini Uganda.

Mpaka sasa idadi ya watu ambao hawajapatikana haijafahamika.

"Naweza kuhakikishia kwamba watu 34 wamefariki, itabidi tusubiri uchunguzi wetu ukamilike tuweze kusema kwa uhakika idadi ya watu ambao bado hawajapatikana" alisema msemaji wa shirika la msalaba mwekundu Bi Irene Nakasiita.

Alhamisi iliyopita alionyesha baadhi ya picha ya kitu ambacho alikielezea kama maporomoko makubwa ya udongo kupitia WhatsApp katika picha hizo pia zilionekana maiti ambazo zimezama kwenye matope pembeni ya mto.

Baadhi ya miili ilikuwa imefunikwa kwa  majani ya migomba na wanakijiji

"Sababu ya maporomoko haya ilikuwa ni baada ya mto kufurika kutokana na mvua kubwa kunyesha. Wakati maji yalipotoka mtoni na kuanza kumiminika yalisomba mawe makubwa na kuharibu nyumba za watu"alisema Nakasiita.

" Timu zetu za uokoaji na utafutaji bado zipo katika eneo la tukio zikiondoa watu katika eneo hilo na kuwatoa kutoka katika kifusi" alisema

Nakasiita pia alisema kwamba shirika la msalaba mwekundu limetuma vifaa mbalimbali kama maturubai, mablanket na dawa za kusafishia maji ya kunywa.

Nathan Tumuhanye ambae ni mkurugenzi wa shirika la kusaidia watu walikumbwa na majanga ya asili na migogoro aliiambia AFP kwamba vijiji vinne na shule moja ya msingi vimeathiriwa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliandika katika mtandao wa Twitter "Nimepokea habari za kusikitisha za maporomoko ya udongo yaliyosababisha uharibifu mkubwa na kuuwa idadi ya wakazi ambao bado haijafahamika. Serikali imetuma timu za uokoaji katika eneo la tukio"

"Serikali itaangalia njia ambazo zipo zinazoweza kutumika kuzuia majanga kama haya yasijirudie"

Wilaya ya Bududa ipo karibu na mlima Elgon katika mpaka wa Uganda na Kenya, ni eneo ambalo lipo katika hatari kubwa ya kukumbwa na maporomoko ya udongo.

Mnamo mwezi wa tatu mwaka 2010 maporomoko ya udongo yaliuwa watunzaidi ya 100 katika wilaya hii ya Bududa, na mwaka 2012 maporomoko yaliharibu vijiji vitatu.

Juhudi za serikali kuwahamisha watu kutoka eneo hili zimegonga mwamba kutokana na wakazi wa eneo hili kugoma.

Kwa mujibu wa Tumuhamye walianzisha mfumo wa kuwajulisha watu uwezekano wa kutokea  mafuriko katika eneo hilo lakini bila uwezo wa kuitikia maonyo hayo, haikuwasaidia watu kuokoka kutoka katika majanga haya.

 

 

 Habari Zinazohusiana