Ebola yadhibitiwa katika kitovu chake Jamhuri ya Kidemokrsaia ya Kongo

Serikali  ya JK Kongo yafahamisha kudhibiti Ebola katika kitovu chake baada ya kusababisha vifo vya watu zaidi ya 80

Ebola yadhibitiwa katika kitovu chake Jamhuri ya Kidemokrsaia ya Kongo

Waziri wa afya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  Oly Ilunga amefhamisha Jumapili kuwa Ebola imethibitiwa katika kitovu chake ambapo  watu zaidi ya 80 wamefariki kutokana  na virusi vya ebelo tangu kulipuka kwake kwa mara nyingine Agosti Mosi.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na wizara ya afya,  kitovu cha Ebola  Beni Mashariki mwa JK Kongo  watu zaidi ya 80 wamefariki dunia kutokana na virusi  hivyo hatari.

Kwa mara ya kwanza kkesi ya virusi hivyo iligunduliwa Mangine eneo ambalo linapatikana katika umbali wa kilomita  zaidi ya 30 na mji wa Beni.

Licha ya kufahamishwa kudhibitiwa virusi hivyo, waziri wa afya ametolea wito  raia katika eneo hilo kuwa waangalifu.Habari Zinazohusiana