Rais  wa Madagascar ajiuzulu

Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina ajiuzulu ili kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu Novemba

Rais  wa Madagascar ajiuzulu

Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina amefikisha waraka wake wa kujiuzulu Ijumaa katika ofisi  kuu za  baraza la mahakma ya katiba nchini Madagascar. 

Taariha iyo imetolewa  hapo Ijumaa na  baraza la katiba  katika  tovuti yake.

Hery Rajaonarimampianina  amelazimika kujiuzulu  kama wanavyofahamisha  wadadisi wa masuala ya kisiasa kuwa anataraji kuwania kwa mara nyingine kiti cha urais katika uchaguzi mkuu nchini Madagascar.

Uchaguzi mkuu nchini Madagascar unatarjiwa kufanyaika ifikapo Novemba 7.

Kipengele cha katiba   katika kifungu  cha 46 kinasema kuwa rais alie madarakani  iwapo atataraji kuwania kiti cha urais anatakiwa  kujiuzulu  siku 60 kabla ya tarehe iliopangwa kufanyka uchaguzi.

Wangombea 46 walijiandisha kugombea kiti cha urais huku tume ya uchaguzi imetangaza kupasisha   wagombe 36 wakiwemo marais watatu wa zamani  wa nchi hiyo.

 Habari Zinazohusiana