Upinzani waingia katika bunge nchini Rwanda

Upinzani waingia katika bunge baada ya uchaguzi  uliofanyika  Jumatatu nchini Rwanda

Upinzani waingia katika bunge nchini Rwanda

Kulingana na matokeo ya muda  baada ya uchaguzi wa wabunge ulifanyika nchini Rwanda Jumatatu, chama cha upinzani  cha PVDR kimepata asilimia 5 ya kura na kujishindia viti viwili  bungeni.

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Rwanda chama cha upinzani kuingia bungeni kulingana matokeo ya  muda ya uchaguzi uliofanyika  Jumatatu.

Chama cha PVDR  ambacho kinaongozwa na Frank Habineza  kimeshinda vitiviwili  katika bunge ambalo lina viti 80.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo  yatatolewa Septemba 16. Raia takribani milioni 7  wamewachagua wabunge watakao wawakilisha. 

Uchaguzi huo ni uchaguzi wa 4  kufanyika nchini Rwanda tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari  ya mwaka 1994.

Chama cha PDVR  kiliundwa  mwaka 2009 na kiongoni wake Habineza aliwania kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2017 na kupata asilimia 0,47 ya kura.Habari Zinazohusiana