Marais wa mataifa ya Afrika ya Kati na Kusini kukutana mjini Luanda nchini Angola

Marais wa mataifa ya Afrika ya Kati na Kusini kukutana mjini Luanda nchini Angola Agosti 14

Marais wa mataifa ya Afrika ya Kati na Kusini kukutana mjini Luanda nchini Angola

Marais wa mataifa ya Afrika ya Kati na Kusini kukutana mjini Lunda nchini Angola ifikapo Agosti 14.

Taarifa kuhusu mkutano huo imetolewa na Ijumaa na waziri wa mambo ya nje wa Angola Manuel Augusto.

Waziri wa mambo ya nje wa Angolo amesema kwamba katika mkutano huo kutazungumzia  hali ya kisiasa katika  ukanda na mbinu za kutatua mizozo inayojitokeza.

Vile vile katika mkutano huo kutazungumziwa kuhusu ushirikiano  katika biashara na kuwavutia wawekezaji nchini Angola.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, rais wa Kongo, rais wa Afrika Kusini, rais wa Rwanda, Uganda , Gabon na Moussa Faki Mahamat ni miongoni mwa viongozi  wanaotarajiwa kushiriki katika mkutano huo.

Mkutano huo utaongozwa na rais wa Angola Joao Lourenco.

 Habari Zinazohusiana