Kuapishwa kwa rais kwaahirishwa nchini Zimbabwe

Sherehe za kuapishwa kwa rais zilizokuwa zimepangwa kufanyika Jumapili zimeahirishwa nchini Zimbabwe

Kuapishwa kwa rais kwaahirishwa nchini Zimbabwe

Sherehe za kuapishwa kwa rais zilizokuwa zimepangwa kufanyika Jumapili zimeahirishwa nchini Zimbabwe.

Hii ni kufuatia upinzani kuyapinga kihalali matokeo ya uchaguzi mkuu.

Katika  uchaguzi mkuu uliopita Emmerson Mnangagwa alitangazwa mshindi baada ya kupaya asilimia 50.8 ya kura huku Nelson Chamisa wa chama cha NDC akiwa na asilimia 44.3.

Chama cha MDC kimeyapinga matokeo hayo na kusema kuwa uchaguzi wa Julai 30 ulikuwa na udanganyifu.

Wiki iliyopita wafuasi wa chama cha upinzani walifanya maandamano yaliyopelekea vifo vya watu sita.

Mwanasheria wa MDC Thabani Mpofu amesema kuwa mahakama ina siku kumi na nne kuamua kama kuapishwa huko kutaendelea ama la.Habari Zinazohusiana