Rais Joseph Kabila amteua Emmanuel Ramazani kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu JK Kongo

Rais Joseph kabila amteua Emmanuel Ramazani kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

kabila.png
Emmanuel-Ramazani.jpg

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amteua Emmanuel Ramazani Shadary kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo ifikapo Disemba 23 mwaka 2018.

Emmanuel Ramazani ni katibu wa chama  tawala  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika mkutanao na waandishi wa habari msemaji wa serikali Lambert Mende  Jumatano amefahamisha kuwa  Rais Joseph Kabila amemteua Emmanuel Ramazani kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Kabla ya kuteuliwa kuwa mkombea katika uchaguzi huo, Shadary  alikuwa  naibu waziri mkuu alihusika na mambo ya  ndani ikiwemo usalama.

Shadary  ni mzawa wa Maniema , Mashariki mwa Jamhuri  ya Kidemokria ya Kongo ambapo alikuwa gavana  kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2001.

 Habari Zinazohusiana