Vifo kutokana na Ebola vyaongezeka DRC

Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa Ebola vimeongezeka mpaka kufikia 23 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Vifo kutokana na Ebola vyaongezeka DRC

Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa Ebola vimeongezeka mpaka kufikia 23 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Katika taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), imeelezwa kuwa kesi 44 zimegunduliwa tangu 4 Aprili katika maeneo ya Bikoro, Iboko, Wangata na Mbandaka.

Toka kutolewe kwa ripoti hiyo,kwa mara ya kwanza tangazo la kuitahadhari jamii limetolewa.

Timu ya dharura imetumwa Kaskazini Magharibi kusaidia kuenea kwa janga hilo.

WHO imetuma vifaa  na dozi 4000 za chanjo ya Ebola katika maeneo tofauti nchini humo.

 

 


Tagi: Ebola DRC , vifo

Habari Zinazohusiana