Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika akemea mauaji ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika akemea mauaji ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika akemea mauaji ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza

Musa Faki Muhammed, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika akemea mauaji ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza katika maandamano yaliofanyika Jumatau kupinga uamuzi wa Marekani na kufunguliwa kwa ubalozi wake mjini Yerusalamu. Watu 59 wamefariki na wengine zaidi ya 2 500 wamejeruhiwa.

Umoja wa Afrika umelaani mauaji yaliotekelezwa na jeshi la Israel katika maandamano yaliaofanyika ukanda wa Gaza kupinga ufunguzi wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu.

Musa Faki Muhammed amelaani kitendo cha jeshi la Israel  kutumia silaha za moto dhidi ya waandamanaji na kupelekea vifo vya watu 59.

Umoja wa Afrika umetolea wito jumuiya  ya kimataifa kupatia ufumbuzi mzozo wa Palestina ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 50.

 Habari Zinazohusiana