Afrika Kusini yamuondoa balozi wake Israel

Serikali ya Afrika Kusini yamtoa balozi wake mjini Tel Aviv na kuamtaka arejee nchini kufuatia ghasia na uamuzi wa Marekani kuhamisha ubalozi wake mjini Yerusalemu

Afrika Kusini yamuondoa balozi wake Israel


Afrika Kusini imechukuwa uamuzi wa kumtoa balozi wake Israel kutoka na mauaji ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza ambapo watu 59 waliuawa  na wengine zaidi ya 2300 kujeeuhiwa.
Umuzi huo umechukuliwa na Afrika kama ishara ya kukemea madhila ya wapalestina , mauaji na ghasia zinazoendelea.

Katika tamko lililotolewa na balozi wa Afrika Kusini Sisa Ngobane limefahamisha kuwa Afrika Kusini inatolea wito jeshi la Israel kuacha kushambulia wapalestina katika ardhi yao bamoja na Ukanda wa Gaza.
Vile tamko hilo limelitaka jeshi la Isarel  kuondoka katika maeneo ya  wapalestina.Habari Zinazohusiana