Zaidi ya watoto 1000 wametekwa na Boko Haram nchini Nigeria

Shirika UNICEF limesema kuwa ni zaidi ya watoto 1000 wametekwa na Boko Haram huku mamilioni wakiwa wamehamishwa makazi yao Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Baada ya tukio la utekaji wa wanafunzi 276,UNICEF imesema kuwa matukio kama hayo yanaharibu mustakabali wa elimu na maisha ya watoto.

Mpaka sasa ni watoto 112 bado wametekwa na kundi hilo na utekaji huo unaonekana kupamba moto jinsi siku zinavyozidi kusonga mbele.

Kwa mujibu wa habari,watoto wamekuwa wakitekwa na kuteswa katika mahala tofauti ikiwemo mashuleni.

Tangu mgogoro ulipoanza kaskazini mashariki mwa Nigeria karibu miaka tisa iliyopita, angalau walimu 2,295 wameuawa na shule zaidi ya 1,400 zimeharibiwa.

Shule nyingi zimeshindwa kufunguliwa na kuendelezwa kutokana na kutokuwa na usalama.

 Habari Zinazohusiana