Watu 16 wafariki na wengine 140 wajeruhiwa kwa kupigwa na radi nchini Rwanda

Watu 16 wafariki na wengine   zaidi ya 140 wajeruhiwa kwa kupigwa na radi Nyaruguru nchini Rwanda

Watu 16 wafariki na wengine 140 wajeruhiwa kwa kupigwa na radi nchini Rwanda


Meya wa Nyaruguru François Habitegeko amewaambia waandishi wa habari  radi iliopiga kanisa moja katika eneo hilo imesababisha vifo vya watu  16 na kuwajeruhi wengine 140.

Tukio hilo lililtokea Jumapili.

Majeruhi wa tukio hilo walipelekwa hospitali wakiwa katika hali mbaya baada ya kupigwa na radi.

Kwa mujibu wa taarifa zizlitolewa na runinga ya taifa nchini Rwanda, kanisa hilo halikuwa na mfumo wa kujilinda na radi.

Mvua kali na mingurumo ya radi  Rusenge ilipelekea  wanafunzii 18 kujeruhiwa na mmoja kufariki.


Tagi: Rusenge , Radi , Rwanda

Habari Zinazohusiana