Wanafunzi watano wafariki na wengine 43 wajeruhiwa katika mlipuko wa bomu Tanzania

Wanafunzi watano wafariki na wengine 43 wajeruhiwa baada ya bomu la kurushwa kwa mkono kulipuka Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania

Wanafunzi watano wafariki na wengine 43 wajeruhiwa katika mlipuko wa bomu Tanzania

 

Wanafunzi watano  wamefariki na wengine 43 wajeruhiwa  akiwemo mwalimu mmoja baada ya bomu la kurushwa kwa mkono kulipuka.

Tukio hilo limetokea Jumatano katika shule ya msingi ya Kihinga inayopatikana Ngara Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania.

Kamanda wa jeshi la Polisi Augustine Ollomi  amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa  wanafunzi  watatu walifariki wakati wa tukio na wengine wawili walifariki wakiwa katika hospitali ya Rulenge.

Kamanda huyo wa Polisi alisema kuwa  baada ya uchunguzi ilidhihirika kuwa mwanafunzi mmoja aliokota bomu hilo na kuingia nalo darasani.Habari Zinazohusiana