Uturuki imekuwa muhimu sana kwa taifa la Somalia

Mbunge wa Somalia amempongeza sana rais Erdoğan kwa kazi nzuri na msaada mkubwa anaoonyesha kwa taifa la Somalia.

Uturuki imekuwa muhimu sana kwa taifa la Somalia

Mbunge mmoja wa Somalia amempongeza sana rais Erdoğan kwa kazi nzuri na msaada mkubwa anaoonyesha kwa taifa la Somalia.

Kwa mujibu wa habari,mbunge huyo ameyasema hayo wakati alipohudhuria mkutano wa Pan Africa nchini Afrika Kusini.

Bwana Sherif Mohamed pia amesema kuwa Somalia ilivutiwa sana na Uturuki hasa pale rais Erdoğan aliposhuka ndege na kwenda moja kwa moja kuwatizama wanyonge nchini Somalia.

Uturuki imekuwa ikitoa msaada mkubwa Somalia toka kipindi ambacho rais Erdoğan alikuwa bado ni waziri mkuu.

Uturuki imejenga kambi kubwa ya kijeshi kwa lengo la kulijega na kuliimarisha jeshi la Somalia.Habari Zinazohusiana