Sudan yaruhusu msafara wa misaada kuingia Sudan Kusini

Serikali ya Kharthoum yaruhusu msafara wa misaada ya kiutu kuingi nchini Sudan Kusini

Sudan yaruhusu msafara wa misaada kuingia Sudan Kusini

 

Serikali ya Kharthoum yaruhusu msafara wa misaada ya kiutu kuingi nchini Sudan Kusini

Naibu mtendaji  katika kamishna ya utoaji misaada wa Sudani Kusini  amefahamisha hapo Jumatano kuwa serikali ya Khartoum ameruhusu misafara ya misaada ya kiutu kuelekea kuingia nchini Sudan Kusini.

Misaada ya kiutu kutoka katika shirika la Umoja wa Mataifa la WFP itawafikia walengwa nchini humo.

Uongozi wa Sudan Kusini umepongeza  hatua ya Khartoum na kusema kuwa  utarahisisha usafiri wa tani 1000 za chakula  katika eneo ambalo limekumbwa na uhaba wa chakula na utapi wa mlo.

Khartoum alifunga mpaka wake na Sudan Kusini mwaka 2011 kwa madai kuwa Juba inatoa hifadhi kwa waasi  wanaoshambulia Sudan.


Tagi: UN , WFP , Sudan Kusini , Sudan

Habari Zinazohusiana