31 wahukumiwa adhabu ya kifo nchini Misri

Watu 31 wamepewa adhabu ya kufa kufuatia mauaji ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2015 nchini Misri

31 wahukumiwa adhabu ya kifo nchini Misri

Mahakama moja nchini Misri siku ya Jumamosi ilitoa hukumu ya kifo kwa watuhumiwa 31 kwa mashtaka ya kuhusika na mauaji ya mwendesha mashtaka mkuu mmoja nchini humo mwaka 2015.

Hisham Barakat,alikuwa mwendesha mashtaka mkuu aliyeuawa katika shambulizi la bomu lililotegwa katika gari akiwa na wajumbe wake mashariki mwa Cairo mnamo Juni 2015.

Watuhumiwa hao 31 ni miongoni mwa watu 68 wanaodaiwa kushiriki katika kupanga shambulizi hilo .

Watu hao 31 wamepewa adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya kutekeleza mauaji,kuhusika na kundi la kigaidi,na pia kupatikana na slaha hatari na pia vilipuzi.

Mamlaka nchini Misri pia imetuhumu kundi la Muslim Brotherhood nchini humo na lile la Hamas la Palestina kuhusika na shambulizi hilo madai ambayo makundi yote mawili yamekataa kabisa kuwa na uhusiano nayo.

Barakat ni kiongozi wa ngazi za juu nchini humo kuuawa tangu mapinduzi ya mwaka 2013 dhidi ya serikali ya Mohammed Morsi.

 

 Habari Zinazohusiana