Mtoto wa Gaddafi aachiliwa huru

Mtoto wa aliekuwa kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi aachiliwa huru

Mtoto wa Gaddafi aachiliwa huru

 

Mtoto wa aliekuwa kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi aachiliwa huru

Mtoto wa Muamar Gaddafi, Seif al Islam aachiliwa huru na kikundi cha wapiganaji kilichokuwa kimemkamata kwa muda mrefu tangu kuanza kwa machafuko nchini Libya.

Taarifa zilizotolewa na kundi moja la wapiganaji Zenten Jumamosi Juni 10 zilifahamisha kuachiwa huru kwa Seif al Islam Gaddafi aliekuwa akishikiliwa tangu Novemba mwaka 2011.

Mawakili watetezi wa Seif al Islam walifahamisha kuwa mteja wao alinufaika na sheria iliowekwa mwaka uliopita ambayo ilikuwa bado haijatekelezwa kwa viongozi wa ngazi za juu wa Libya.

Kundi la  Abu Baqr al-Sadiq lilitangaza Ijumaa kumuacha huru Seif al Isalm.

Licha ya kuacha huru nchini Libya Seif al Islam anasakwa na mahakama ya kimataifa ya haki za binadamu.Habari Zinazohusiana